Tarehe 20 Desemba 2024, tulipata heshima kubwa ya kupokea ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb), katika kiwanda chetu kilichopo Kayenze Ndogo.

Ziara hii ilikuwa fursa muhimu ya kuonesha jinsi tunavyoboresha sekta ya uvuvi kupitia teknolojia bunifu. Mheshimiwa Waziri alishuhudia kwa karibu jinsi tunavyotumia taa za umeme wa jua kwa uvuvi pamoja na mbinu za kisasa za ukaushaji wa dagaa, ambazo zinachangia kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi huku tukihifadhi mazingira.

Tunashukuru sana kwa mwongozo na sera madhubuti zinazotolewa na serikali katika kuendeleza sekta ya uvuvi na mifugo. Tukiwa mstari wa mbele katika uvumbuzi na maendeleo endelevu, tutaendelea kuchangia katika kuboresha maisha ya jamii zinazotuzunguka na kukuza uchumi wa sekta hii muhimu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *